Luke 4

Yesu Ajaribiwa Na Shetani

(Mathayo 4:1-11; Marko 1:12-13)

1 aYesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi nyikani, 2 bmahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula chochote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.

3 cIbilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”

4 dYesu akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ”

5 eIbilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja. 6 fAkamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka. 7Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”

8 gYesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”

9 hKisha ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, 10 ikwa maana imeandikwa:

“ ‘Atakuagizia malaika zake
ili wakulinde;
11 jnao watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”
12 kYesu akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

13 lIbilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Yesu mpaka wakati mwingine ufaao.

Mwanzo Wa Huduma Ya Galilaya

(Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15)

14 mKisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. 15 nAkaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.

Yesu Akataliwa Nazareti

(Mathayo 13:53-58; Marko 6:1-6)

16 oYesu akaenda Nazareti, alipolelewa, na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, 17 pnaye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa:

18 q “Roho wa Bwana yu juu yangu,
kwa sababu amenitia mafuta
kuwahubiria maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao,
na vipofu kupata kuona tena,
kuwaweka huru wanaoonewa,
19 na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”
20 rKisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 sNdipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.”

22 tWote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

23 uYesu akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”

24 vYesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. 25 wLakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima. 26 xHata hivyo Eliya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 yPia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu.”
Shamu hapa inamaanisha Syria.


28Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. 29 aaWakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali. 30 abLakini yeye akapita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.

Yesu Atoa Pepo Mchafu

(Marko 1:21-28)

31 acKisha Yesu akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilaya, na katika siku ya Sabato akawa anafundisha. 32 adWakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.

33 aeNdani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Naye akapiga kelele kwa nguvu akisema, 34 af“Tuache! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

35 agBasi Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akisema, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” Yule pepo mchafu akamwangusha yule mtu chini mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru. 36 ahWatu wote wakashangaa, wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!” 37 aiHabari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile.

Yesu Awaponya Wengi

(Mathayo 8:14-17; Marko 1:29-34)

38 ajYesu akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Basi huko alimkuta mama mkwe wa Simoni akiwa ameshikwa na homa kali, nao wakamwomba Yesu amsaidie. 39 akHivyo Yesu akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka saa ile ile, naye akaanza kuwahudumia.

40 alJua lilipokuwa linatua, watu wakamletea Yesu watu wote waliokuwa na maradhi mbalimbali, naye akaweka mikono yake juu ya kila mgonjwa, naye akawaponya. 41 amPepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Kristo.
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


42 aoKesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke. 43 apLakini yeye akawaambia, “Imenipasa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, kwa maana kwa kusudi hili nilitumwa.” 44 aqNaye aliendelea kuhubiri katika masinagogi ya Uyahudi.

Copyright information for SwhNEN